Dec 11, 2012

Je wewe ni mpenzi kusoma vitabu kama mimi?

Bwana Yesu asifiwe...hope hamjambo wapendwa wangu..

Wapendwa mimi ni mpenzi mkubwa wa kusoma vitabu...napendelea zaidi vitabu vyenye kutoa mafunzo mbalimbali ya kimaisha,pia vitabu vinavyowahusu watu mashuhuri duniani ninaowapenda na pia napenda kusoma detective novels...

Ndio kwanza nimemaliza kusoma kitabu cha mzee Mandela kinaitwa LONG WALK TO FREEDOM...Sijutii muda wangu niliotumia kusoma hichi kitabu...
I love Nelson Mandela...nampenda sana huyu baba kila mtu wangu wa karibu ukimuuliza Edina anampenda kiongozi gani hapa duniani watakutajia mzee Mandela...ninakosa raha nikisikia anaugua na mara kwa  huwa namfanyia maombi yakumpatia afya njema...Siku nyingi tokea niko secondary nilikua na ndoto ya kwenda Robben Island kutembelea gereza alilofungwa Mandela kwa miaka 27...Mungu ni mwema mwakan nitakwenda Afrika Kusini kutimiza ndoto yangu hiyo...I cant wait...

Hapa chini ni baadhi ya maneno ya mzee Mandela yaliyonifurahisha na kunifundisha na kunitafakarisha sana ambayo yanapatikana katika hichi kitabu,

''It was during those long and lonely years that my hunger for the freedom of my own people became a hunger for the freedom of all people, WHITE and BLACK. I knew as well as I know anything that the oppressor must be liberated just as surely as the oppressed. A man who takes away another man’s freedom is a prisoner of hatred, he is locked behind the bars of predjudice and narrow-mindedness...''

Pia maneno yafuatayo yanapatikana katika kitabu hichi,

''No one is born hating another person because of the color of his skin, or his background, or his religion. People must learn to hate, and if they can learn to hate, they can be taught to love, for love comes more naturally to the human heart than its opposite''

Nelson Mandela

Nov 28, 2012

GALILAYA WAJA NA HAKUNA KAMA MAMA

 


 

ISAYA MSANGI

Vijana watano wanaounda kundi la muziki wa injili liitwalo Galilaya lililo chini ya mwimbaji wa muziki huo Isaya Msangi limekamilisha albamu yake ya kwanza iitwayo ‘Hakuna Kama Mama’ ikiwa imesheheni vibao vinane.

Akizungumza na TGM jana jijini Dar es Salaam, Msangi ambaye ndiyo mmiliki wa kundi hilo alisema ameamua kuunda kundi hilo kwa lengo la kuongeza nguvu ya kulitangaza neno la Mungu kila pembe ya dunia kwa njia ya uimbaji.
Msangi aliendelea kusema kuwa baadhi ya nyimbo tayari zimeanza kuchezwa katika vituo mbalimbali vya redio na sasa anafanya taratibu za kurekodi video yake.
Alizitaja nyimbo zinazounda albamu hiyo kuwa ni Hakuna Kama Mama, Amenikumbuka Yesu, Maombi, Ukifika Mbinguni, Bendera ya Yesu, Safi Sana, Mbiyo na Tanzania Tunaenda mbele.
“Namshukuru Mungu nimefanikiwa kukamilisha albamu yangu ya kwanza nikiwa na kundi hili ambalo litakuwa linahubiri neno la Mungu kwa njia ya uimbaji,” alisema Msangi na kuongeza;
Lakini kuwa na kundi hili hakuna maana sitaiba peke yangu bali nitakuwa natoa albamu kwa kila upande kadiri Roho wa Mungu atakavyoniongoza.
Mwimbaji huyo ambaye albamu yake ya Shetani Imekula Kwako ikiwa katika mfumo wa video inayofanya vizuri sokoni anatarajia kulizindua kundi hilo hivi karibuni na tayari mchakato wa uzinduzi umeanza.
EDINA SAYS:
Hongera sana rafiki yangu Isaya kwa kuunda kundi la Galilaya na kwa album yenu.
Mungu azidi kukubariki kwa kazi zako nzuri mtumishi.
source:Tanzania Gospel Music.

Nov 26, 2012

Kwanini mtu anaweza kuomba jambo na asijibiwe?.

Katika Yoh14:13 Bwana Yesu anatuahidi kwamba '' Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu,hilo nitafanya,....'
sasa inakuwaje unapiga magoti sana ukifunga na kusali ila Bwana Yesu hatimizi ahadi yake kwako kwa kukupatia lile umuombalo?.

Bwana Yesu asifiwe ndugu zangu mnaonitembelea hapa.

well...ni kweli Bwana Yesu alisema tuombe lolote atatupatia ila mpendwa kuna wakati tunaweza kuomba jambo tusipatiwe...sio kama mungu hasikii maombi hayo...hapana...kuna sababu nyingi za kwanini Mungu anaweza asijibu maombi.

Wakati mwingine ombi linaweza lisijibiwe sababu UNAJARIBIWA ila ukisimama katika imani ipo siku utajibiwa...mfano mzuri ni Sara...Sara hakukata tamaa mwishowe akapewa mtoto akiwa keshazeeka...hebu jiulize ingekua ni wewe ungeweza  kuendelea kumtumainia Mungu au ungekimbilia kwa kalumanzira?.

Vilevile ukisoma katika Yak 4:2-3 utaona kwamba kuna maombi hajibiwi sababu lengo la kinachoombwa halimfurahishi Mungu.Chukulia mfano unamuomba mungu akubariki cheo fulani ambacho kitakusaidia kula rushwa au kujipatia wanawake kirahisi kwa kuwaahidi ajira iwapo watakuhonga ngono.Biblia imeweka wazi kuwa maombi kama haya hayatajibiwa.

Kila tunachomuomba mungu kinatakiwa kiwe na nia safi...Mungu hawezi kukupatia kitu unachomuomba ili ukawakomeshe au unachotaka ili uwanyanyasie jirani zako.

Pia tukumbuke kwamba Mungu ni baba yetu,sisi ni watoto wadogo sana mbele zake,yeye anajua mengi ambayo sisi hatujui hivyo tukimuomba jambo ambalo yeye anaona litatuletea matatizo hatatupatia....sisi tunaweza kumuomba jambo tukidhani ni zuri kumbe yeye kwa macho yake ya kiungu ameona si zuri...kumbuka mtoto wako akikuomba wembe huwezi kumpatia ...hivyo na baba yetu wa mbinguni ni hivyo hivyo.


Ni hayo tu kwa leo wapendwa wangu.
Nakaribisha kukosolewa na kusahihishwa iwapo mtu ataona kuna nililosema lisilo sahihi.


WITH LOVE.
EDINA.
Aug 14, 2012

NIMEKUSAMEHE

Moyo wangu hauna nguvu wala nafasi ya kubeba chuki dhidi ya walionikosea katika maisha yangu yaliyopita.

 Mpendwa je wewe ni mtu ambaye kuna watu wame/likukosea kila ukikumbuka walivyokufanyia unashindwa kuwasamehe?

Kama wewe ni miongoni mwa wasioweza kusamehe ningependa kukufahamisha kuwa unapohifadhi chuki moyoni mwako anayeumia ni wewe.

Mbali ya kuwa kuhifadhi chuki kwa kushindwa kusamehe kunaweza kukuletea  maradhi kama vidonda vya tumbo,depression,magonjwa ya moyo n.k pia  ni chukizo mbele za Mungu.

Kabla hujaendelea kuwawekea vinyongo watu waliokukosea inabidi ujiulize je ni mara ngapi umemkosea Mungu lakini kila ulipotubu alikusamehe na kusahau kabisa?


Wakati mwingine mtu anaweza kuwa yeye ndiye aliyekukosea ila akawa anajitahidi kuwashawishi watu tena kwa machozi juu  LOL kuwa wewe ndiye uliyemkosea ili watu wakuone kuwa wewe ndiye mbaya.Hata watu wa aina hii pia ni wakuwasamehe na kukabidhi kila kitu kwa Mungu.


Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziye mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote." - 1 Wathesalonike 5:15

GOD IS LOVE

Apr 20, 2012

Nyimbo zenye mahubiri adimu...


Napenda saana ujumbe katika wimbo huu.Mpendwa hebu sikiliza kwa makini maneno ya wimbo huu then tafakari.Inasikitisha kwamba waimbaji hatuimbi tena nyimbo zenye kutoboa ukweli kama hizi,tunaimba zile nyimbo zenye maneno ambayo jamii inahitaji kusikia.
Ubarikiwe saana Mtumishi Munishi kwa kuimba bila kujali jamii itachukuliaje mahubiri yako,simamia katika kweli maana ndiyo itakayotuweka huru,

Apr 19, 2012

Ndugu yenu aliyepotea leo ameonekanaHeheee nacheka kwa aibu maana ni muda mrefu saana tokea nimefanya jambo hapa Ushuhuda Wangu.

Kwa kweli ni kwa sababu ya majukumu kuwa mengi.Hata hivyo siku zote mim nasema kwamba kuwa na mambo mengi ya kufanya  yenye kuboresha maisha yetu ni baraka na neema.

Unapokua busy sana kiasi cha kukosa hata muda wa kuwa na marafiki,au kukutana na ndugu na jamaa au pengine hata kushindwa kufanya mambo tunayopenda kufanya inaweza kutufanya tuchukie kuwa busy,nakujiona utafutaji wa maisha unatugeuza watumwa,lakini  siku nilipowafikiria wasomi ambao wanashinda majumbani bila kuwa na cha kufanya kwa kukosa ajira,au wanaotamani kupata mtaji japo waanzishe biashara yakuboresha maisha lakini hawana na hivyo kuishia kukaa majumbani bila cha kufanya au wagonjwa wanaolala majumbani na kushindwa kuhangaikia shughuli zao  roho ya ulalamishi ilinifa na tokea siku hiyo niliona kwamba mimi ni miongoni mwa wabarikiwa maana nimebarikiwa uwezo wa kuwa busy kuhangaikia maisha yangu bila kikwazo chochote.

Haya,tuachane na hayo,sasa umeshajua kwamba nilipotea sio kwamba nilikua na tatizo lolote wala sikuwa mgonjwa.

Leo naomba nikuulize mpendwa yeyote utakayebahatika kufika katika blog hii.

Je mpendwa wangu umeshawahi kuisikia sauti ya Mungu ikizungumza nawe?
Je unaamini kwamba Mungu anazungumza nasi kila mara?
Je unafahamu kwamba,shetani naye ana sauti yake inayojaribu kuzungumza nasi?(b)Utawezaje kuitofautisha sauti ya Mungu na sauti ya shetani?

Mim naisikia sauti ya Mungu,huwa ninaitii na vile vile zinapokuja sauti zingine zisizo toka kwa roho wa Mungu ninazifahamu maana roho wa Mungu aliyeko ndani yangu unisaidia kuzitambua haraka na ninazikemea.

Ni muhimu sana kufahamu jinsi ya kuifahamu na kuisikia sauti ya Mungu.

Kwa leo nitaishia hapa,ila nitafanya muendelezo wa topic hii muhimu ambapo na vifungu vya biblia vitatumika katika kueleweshana jambo hili.

Nawaacha katika mikono salama ya Mungu wetu,Mungu mwenye matendo makuu yasioelezeka na yenye kutisha kama nini.Tungekuje leo kama hangekua mweye huruma,mpole na mwenye kusamehe?

Mbarikiwe!

Oct 10, 2010

tuko safarini usijisahau

Bwana Yesu asifiwe.
inasikitisha kwamba baadhi yetu tunaishi hapa duniani as if tumeshafika mwisho wa safari yetu.
Napenda kuitumia jumapili ya leo kukukumbusha ya kwamba hapa duniani tunasafiri,hapa sio nyumbani kwetu,nyumbani kwetu ni kule alikotangulia Yesu kutuandalia makao.
Tafuta sehemu iliyotulia ukae peke yako uuchunguze moyo wako ili upate kujua ni kitu gani kinachoweza kusababisha usipate kibali cha kuingia kule katika mji wa ahadi ambako ndiko nyumbani kwetu kisha ujiepushe nacho kwani kule nyumbani kwetu hakuna kilicho kinyonge kitakachoingia.
MAY OUR LORD JESUS BE WITH ALL OFF YOU.
THANK YOU.

   msikilize Jím Reeves ushushie kaujumbe kangu.